1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaUjerumani

Ujerumani yatia saini ushirikiano na mataifa ya Asia ya Kati

30 Septemba 2023

Ujerumani imekubaliana juu ya ushirikiano wa kimkakati na mataifa matano ya Asia ya Kati, ushirikiano huo ukijikita katika masuala ya uchumi, nishati, hali ya hewa na mazingira.

https://p.dw.com/p/4WzVc
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akisalimiana na Rais wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akisalimiana na Rais wa Uzbekistan Shavkat MirziyoyevPicha: JOHN MACDOUGALL/AFP

Ujerumani imechukua uamuzi huo ili kukabiliana na ushawishi wa Urusi katika eneo la Asia ya Kati.

Makubaliano hayo yalitiwa saini jana baada ya Kansela Olaf Scholz kuwakaribisha viongozi wa Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan, Turkmenistan na Uzbekistan katika mkutano wa kilele wenye nia ya kuzileta karibu nchi hizo zilizokuwa Jamhuri za zamani za muungano wa Sovieti.

Mkutano huo ulikuwa ni jaribio la kuimarisha uhusiano na mataifa hayo yenye utajiri wa raslimali katikati ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Kulingana na taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano huo wa kilele uliofanyika mjini Berlin, makubaliano hayo ambayo ni ya kwanza ya aina yake, yanalenga kuimarisha ushirikiano ambao umekuwepo kwa miaka 30.