1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Ujerumani yatangaza msaada zaidi wa kibinadamu kwa Gaza

Sylvia Mwehozi
6 Septemba 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema Berlin itaongeza misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza kwa kiasi cha Euro milioni 50.

https://p.dw.com/p/4kKnp
Baerbock akiwa nchini Jordan
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock na mwenyeji wake, waziri wa mambo ya nje wa Jordan Aiman al-SafadiPicha: Soeren Stache/dpa/picture alliance

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema Berlin itaongeza misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza kwa kiasi cha Euro milioni 50. Baerbock ametoa tangazo hilo katika mkutano na waziri wa mambo ya nje wa Jordan Ayman al-Safadi mjini Amman. Baerbock ameongeza kuwa kiasi kilichotolewa na Ujerumani kwa Ukanda wa Gaza tangu mwaka jana ni zaidi ya Euro milioni 360. Misaada hiyo itaelekezwa katika kupambana na njaa, utapiamlo pamoja na utoaji wa huduma za afya. Ujerumani yataka mzozo wa Gaza umalizike

Ujerumani pia itaongeza msaada wa kibinadamu kwa wakimbizi wa Syria walioko Jordan kwa euro milioni 12.7, na kuongeza msaada kwa Jordan hadi Euro milioni 63. Kabla ya safari yake nchini Jordan, Baerbock alitembelea Saudi Arabia na anatarajiwa kuzuru Israel katika ziara yake ya Mashariki ya Kati.