1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yashinikiza amani Sudan

24 Januari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ametoa wito wa kuongeza juhudi ili kuleta suluhisho la vita vya nchini Sudan.

https://p.dw.com/p/4bd7f
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani, Annalena Baerbock.
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani, Annalena Baerbock.Picha: Thomas Imo/photothek/IMAGO

Baerbock ametoa wito huo kabla ya kuanza ziara katika nchi za Afrika Mashariki.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani anakusudia kushirikiana na viongozi wa eneo hilo ili kutafuta njia ya kuwaleta kwenye meza ya mazungumzo majenerali wawili wa pande hasimu za jeshi la Sudan na hivyo kuweza kuwaepusha watu wa Sudan kutumbukia katika maafa makubwa zaidi na pia kuepusha kuliyumbisha zaidi eneo linalopakana na nchi hiyo.

Majenerali hao, Abdel Fattah al-Burhan na mwenzake Mohamed Hamdan Daglo, wamekuwa wanagombea mamlaka tangu mwezi Aprili mwaka uliopita.

Waziri Baerbock anatarajiwa pia kufanya ziara katika nchi za Djibouti, Kenya na Sudan Kusini.