1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yasaidia utunzaji mbuga za wanyama Tanzania

10 Mei 2021

Serikali ya Ujerumani imetoa kiasi cha yuro milioni ishirini kwa ajili ya kusaidia utunzaji wa hifadhi za wanyama pori katika mbuga za Nyerere, Selou na Serengeti nchini Tanzania.

https://p.dw.com/p/3tCTM
Tansania | Deutsche Botschafterin Regine Hess
Picha: DW/H. Bihoga

Hii ni sehemu ya kuendeleza ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili yenye historia ndefu.

Fedha hizo ambazo ni zaidi ya bilioni hamsini za kitanzania zinalengwa kutumika katika kulinda ikolojia pamoja na kuimarisha mahusiano na majirani wanaoishi karibu na hifadhi hizo ambazo ziliwahi kupata tuzo kadhaa za kimataifa kutokana na kuwa na wanyama wa kuvutia wakubwa kama vile Simba, Tembo, na hata Twiga ambao wanaongeza kuvutia watalii.

Fedha zitatumika kulinda ikolojia katika hifadhi 

Akizungumza wakati akikagua miradi mbalimbali balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Regine Hess amesema, janga la virusi vya Corona limeitikisa dunia na sekta ya utalii kwa kiwango kikubwa imeathirika hivyo hakuna budi kuhakikisha jitihada zinafanyaka ili kuendeleza utalii.

Deutschland | Junge Afrikanische Steppenelefanten | Serengeti-Park, Hodenhagen
Tembo katika mbuga ya wanyama ya SerengetiPicha: picture-alliance/dpa/imageBROKER

Balozi Hess amesema fedha hizo zitatumika katika kulinda ikolojia katika hifadhi hizo, ambazo zimekuwepo kwa kipindi kirefu sasa. aliongeza

Mradi huo unaokwenda kwa jina la ufadhili wa dharura katika kulinda na kuhifadhi bioanuwai nchini Tanzania, utatekelezwa na taasisi za serikali ambazo zina dhamana ya moja kwa moja na wanyama pori ikiwemo mamlaka ya uhifadhi nchini TANAPA pamoja na mamlaka ya usimamizi wanyama pori tanzania TAWA.

Miradi itakwenda kwa kipindi cha miaka mitatu

Aidha serikali ya Tanzania imesema miradi ambayo itatekelezwa na fedha hizo ni ya kipindi cha miaka mitatu na mbali na kulinda ikolojia ya hifadhi hizo zitalenga kuimarisha mahusiano baina ya vijiji jirani na mbuga hatua ambayo itapunguza kiwango cha uvunaji haramu wa wanyama hao pori.

Afrikas Nationalparks
Punda milia pamoja na nyati wakiwa SerengetiPicha: picture-alliance/dpa/K. Wothe

Waziri wa utalii Damas Ndumbalo amesema miradi iliotolewa fedha hizo itakwenda kwa kipindi cha miaka mitatu na kisha watafanya tathmini ya pamoja kuangalia mafanikio yaliofikiwa.

Itakumbukwa Ujerumani imekuwa mshirika mkubwa wa tanzania na kwa muda mrefu katika kulinda na kuhifadhi wanyamapori, ambapo katika kipindi cha miaka mitano hivi karibuni zaidi ya euro milioni 106 sawa na zaidi ya shilingi za tanzania bilioni 300 zimetolewa katika kuunga mkono juhudi hizo.