1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yajiunga na Kamandi ya Umoja wa Mataifa, UNC

2 Agosti 2024

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani, Boris Pistorius, anasema nchi yake ndiye mwanachama mpya wa Kamandi ya Umoja wa Mataifa nchini Korea Kusini, UNC, inayoongozwa na Marekani.

https://p.dw.com/p/4j3JO
Waziri wa Ulinzi wa Shirikisho la Korea Kusini Pistorius atembelea Kamandi ya Umoja wa Mataifa
Waziri wa Ulinzi wa Shirikisho la Korea Kusini Pistorius atembelea Kamandi ya Umoja wa MataifaPicha: Soeren Stache/dpa/picture alliance

Pistoriusamesema kuwa sasa Ujerumani inalenga kuchangia katika uthabiti wa kanda hiyo. Waziri huyo wa ulinzi ameongeza kuwa Berlin itajadiliana na washirika wa kamandi hiyo katika kambi ya kijeshi ya Pyeongtaek, jinsi inavyoweza kutoa mchango wake kama mwanachama wa 18. Kamandi hiyo ya Umoja wa Mataifa ina jukumu la kuhakikisha kwamba maelewano ya usitishwaji wa mapigano wakati wa vita vya Korea vilivyofanyika kati ya mwaka 1950 na 1953 yanafuatwa.