1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiUjerumani

Ujerumani yaanza kuwarejesha nyumbani raia wa Afghanistan

30 Agosti 2024

Ujerumani imewarejesha nyumbani raia wa Afghanistan, ikiwa ni mara ya kwanza tangu Agosti 2021 tangu kundi la Taliban kurejea madarakani.

https://p.dw.com/p/4k6Y0
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Henning Kaiser/REUTERS

Ndege ya kwanza ya Qatar imeondoka mapema leo katika uwanja wa ndege Leipzig, ikiwa na raia 28 wa Afghanistan wanaotuhumiwa kwa uhalifu na waliotoka katika majimbo mbalimbali ya Ujerumani, kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya jimbo la Saxony.

Waziri wa Mambo ya Ndani Nancy Faeser ameiita hatua hiyo kuwa ni suala la usalama wa Ujerumani, huku kukiwa na mjadala mkali wa kisiasa kuhusu sheria za maombi ya hifadhi na watu kurejeshwa nchi wanazotoka.

Soma pia:Ujerumani yamtimua mkuu wa kituo cha Iran

Ujerumani haina uhusiano wa kidiplomasia na Taliban, na kwa maana hiyo mchakato huo umefanikishwa kwa kuhusisha njia nyingine.