1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yatangaza sheria kali za umiliki wa silaha

29 Agosti 2024

Serikali ya Ujerumani imekubali kuimarisha udhibiti wa silaha, ili kukabiliana na uhamiaji usio wa kawaida na kuchukua hatua nyingine kukabiliana na kitisho cha ugaidi wa itikadi kali za Kiislamu.

https://p.dw.com/p/4k46K
Berlin PK Faeser | Vorstellung Sicherheitspaket nach Anschlag von Solingen
Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Hatua hiyo imetangazwa leo baada ya shambulizi baya la kisu mwishoni mwa juma katika mji wa Solingen.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Nancy Faeser amesema marufuku iliyopo ya kubeba kisu hadharani itaongezwa, na msaada wa kijamii kwa baadhi ya watu wanaotafuta hifadhi ambao walijiandikisha awali kwenye nchi nyingine za Umoja wa Ulaya, yatapunguzwa.

Mtuhumiwa wa shambulizi la Solingen ni raia wa Syria aliyetambuliwa na maafisa wa polisi kama Issa AI H, alitakiwa kupelekwa Bulgaria kutoka Ujerumani mwaka uliopita, lakini aliendelea kubakia nchini. Kundi linalojiita Dola la Kiislamu lilikiri kuhusika na shambulizi hilo.