1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani: Watu 6 wajeruhiwa baada ya kushambuliwa kwa kisu

31 Agosti 2024

Watu watano wamejeruhiwa vibaya hapo jana usiku baada ya kushambuliwa kwa kisu katika mji wa Siegen, magharibi mwa Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4k7mj
Siegen | Shambulio la kisu kwenye basi lajeruhi watu 6
Siegen | Shambulio la kisu kwenye basi lajeruhi watu 6Picha: Rene Traut/IMAGO

Polisi imemkamata mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 32 anayeshukiwa kuwajeruhi watu hao walipokuwa kwenye basi na imesema hakuna dalili zozote kuwa hilo ni tukio la kigaidi.

Shambulio hili linakuja wakati Ujerumani bado inaomboleza vifo vya watu watatu kufuatia shambulio jingine la kisu huko Solingen takriban wiki moja iliyopita.

Soma pia: Ujerumani yatangaza sheria kali za umiliki wa silaha

Waziri wa Mambo ya ndani wa Ujerumani Nancy Faeser alitangaza siku ya Alhamisi marufuku ya kubeba visu kwenye mikusanyiko ya watu wengi na katika usafiri wa masafa marefu.