1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na Afrika Kusini kuimarisha ushirikiano

Sylvia Mwehozi
28 Juni 2023

Ujerumani na Afrika Kusini zinataka kutanua ushirikiano baina yao, kwa mfano katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, licha ya tofauti za kimtazamno kuhusu namna ya kushughulika na Urusi.

https://p.dw.com/p/4T9tl
Nigeria | Rückgabe der Benin-Bronzen in Abuja
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock.Picha: Annette Riedl/dpa/picture alliance

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock na mwenzake wa Afrika Kusini Naledi Pandor wamesisitiza umuhimu wa uhusiano kati ya mataifa hayo mawili katika mji mkuu wa Afrika Kusini Pretoria jana Jumanne.

Kwa upande wake, Pandor amezungumzia miongoni mwa mambo mengine, ushirikiano kwa ngazi ya uchumi, katika utalii na katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na janga la Uviko-19.

Ujerumani imekosoa hasa msimamo wa Afrika Kusini wa kutokemea uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Afrika Kusini ilijitangaza kuwa taifa lisiloegemea upande katika mzozo huo.