1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock kuzungumza na Pandor kuhusu Ukraine

27 Juni 2023

Miongoni mwa mada za mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock, na mwenzake wa Afrika Kusini, Naledi Pandor, ni sera ya Afrika Kusini juu ya Urusi katika muktadha wa uvamizi wake Ukraine.

https://p.dw.com/p/4T6gQ
Außenministerin Annalena Baerbock besucht Südafrika
Picha: Christoph Soeder/dpa/picture alliance

Baerbock aliwasili nchini Afrika Kusini siku ya Jumatatu (Juni 26) kwa lengo la kuendeleza juhudi za kuvimaliza vita vya Ukraine iliyovamiwa na Urusi.

Hata hivyo, mikutano iliyopangwa kufanyika mjini Cape Town iliahirishwa kutokana na Waziri Baerbock kulazimika kuhudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya uliojadili uasi wa kundi la mamluki la Wagner.

Baerbock anataka kutilia mkazo jinsi Afrika Kusini inavyoweza kuongeza uzito wake kwenye kuuunga mkono Mkataba wa Umoja wa Mataifa jambo ambalo linaweza kuifanya Urusi ikomeshe vita vyake dhidi ya Ukraine.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock (kushoto) na mwenzake wa Afrika Kusini, Naledi Pandor.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock (kushoto) na mwenzake wa Afrika Kusini, Naledi Pandor.Picha: Christoph Soeder/dpa/picture-alliance

Afrika Kusini, kwa upande wake, imesisitiza uhusiano mzuri kati yake na Urusi na imepitisha sera ya kutoegemea upande wowote katika swala la vita vya Ukraine.

Viongozi wa Afrika Kusini wanakumbuka jinsi Umoja wa Kisovieti ulivyowaunga mkono wakati wa mapambano yao dhidi ya serikali ya Wazungu wachache wabaguzi wa rangi.

Soma:Afrika Kusini yasifia ujumbe wa amani Ukraine baada ya mazungumzo

Putin aalikwa mkutano wa BRICS

Rais Vladimir Putin wa Urusi amealikwa kuhudhuria mkutano wa kilele wa nchi za BRICS ambazo ni Brazil, India, China na mwenyeji Afrika Kusini utakaofanyika mwezi Agosti kuanzia tarehe 22 hadi 24.

Hii ni hata baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kutoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa Putin kwa tuhuma za uhalifu wa kivita.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.Picha: Pavel Bednyakov/RIA Novosti/AP/dpa/picture alliance

Afrika Kusini ni mwanachama wa Mkataba wa ICC na hivyo inamaamnisha Putin anaweza kukamatwa akikanyaga nchini humo, ingawa nchi hiyo bado haijawekwa wazi msimamo wake kuhusiana na hilo.

Wakati wa ziara yake nchini Afrika Kusini, Baerbock pia atahudhuria mkutano wa tume ya nchi mbili iliyoundwa na Ujerumani na Afrika Kusini mnamo mwaka 1996.

Tume hiyo hukutana kila baada ya miaka miwili na mara hii inatazamiwa kujadili kwa kina masuala ya nishati safi na mafunzo ya kuongeza ujuzi  baina yao.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani alisema nchi yake inaunga mkono jitihada za Umoja wa Afrika za kutaka kuwa mwanachama wa kundi mataifa ya G20.

Vyanzo: DPA/DW