1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Uingereza yapiga kura huku wapinzani wakitarajia ushindi

4 Julai 2024

Vituo vya kupigia kura kote Uingereza vilifunguliwa mapema Alhamis huku kura za maoni zikiashiria chama cha mrengo wa kushoto cha Labour kiko mbioni kupata idadi kubwa ya kura na kuunda serikali mpya

https://p.dw.com/p/4hqzK
Großbritannien | Wahlen Schild Wahllokal in London
Chama cha Labour kiko mbioni kupata ushindi mkubwa na kuunda serikali mpya baada ya miaka 14 ya kuwa katika upinzaniPicha: Jakub Porzycki/NurPhoto/picture alliance

Mamilioni ya wapiga kura wanatarajiwa kushiriki katika zoezi hilo linalotarajiwa kukamililka mwendo wa saa nne usiku.

Soma pia: Starmer atabiriwa kumbwaga Sunak uchaguzi Uingereza

Matokeo ya awali yatakayochapishwa muda mfupi baada ya vituo kufungwa saa nne usiku yatatoa taswira ya kwanza ya jinsi uchaguzi ulivyofanyika katika ngazi ya kitaifa.

Viongozi wa vyama wametoa wito wao wa mwisho kwa wapiga kura baada ya kuzuru nchi hiyo tangu kuitishwa kwa uchaguzi huo.

Waziri mkuu Rishi Sunak amesema kuwa leo inawakilisha "wakati muhimu'' kwa mustakabali wa nchi hiyo huku akidai kuwa chama cha Labour kitatumia uwezo wake "usiodhibitiwa" kuongeza kodi iwapo kitapata wingi wa kura.