1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sunak asema mtazamo kuhusu uhamiaji Ulaya ´umebadilika´

15 Juni 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amesema "mtizamo" kuhusu sheria za uhamiaji barani Ulaya umebadilika na kwamba miito inaongezeka kutaka kanda ya Ulaya kuchukua hatua kali zaidi kuwadhibiti wahamiaji wasio na vibali.

https://p.dw.com/p/4h48b
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi SunakPicha: Ian Forsyth/Getty Images

Akizungumza hapo jana katika siku ya mwisho ya mkutano wa kilele wa kundi la mataifa tajiri ya G7 uliokuwa unafanyika nchini Italia, Sunak amesema viongozi wa kundi hilo wamekubaliana kushughulikia mzizi wa tatizo la uhamiaji haramu.

Katika tamko la mwisho la mkutano huo, viongozi wa mataifa ya Uingereza, Marekani, Ujerumani, Canada, Japan, Ufaransa na Italia wamesema wanazindua muungano wa pamoja wa kupambana na uhamiaji na kutumia fursa zitokanazo na tatizo hilo.

Sunak amesema ishara zinaonesha fikra kuhusu uhamiaji zinabadilika barani Ulaya akitolea mfano tamko la nchi 15 za bara hilo lililotolewa mwezi uliopita kuutaka Umoja wa Ulaya kuongeza makali ya sera zake za kupambana na uhamiaji.