1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UK na EU zapiga hatua katika biashara na Ireland Kaskazini

25 Februari 2023

Uingereza na Umoja wa Ulaya zinakaribia kufikia makubaliano ya kuzifanyia mabadiliko kanuni za biashara za baada ya Brexit zitakazofanya kazi huko Ireland Kaskazini.

https://p.dw.com/p/4NykI
Irland Dublin neuer Premier Leo Varadkar
Picha: Brian Lawless/PA/dpa/picture alliance

Hilo limedokezwa hii leo na waziri mkuu wa Ireland leo Varadkar ingawa amesema bado ni mapema kutabiri iwapo mkataba utapatikana ndani ya siku chache zinazokuja. 

Mfalme Charles wa Tatu aapa kuendeleza mchakato wa amani wa Ireland Kaskazini

Hivi karibuni kumekua  na mwelekeo wa kutia moyo unaolenga kupunguza ukaguzi mkali wa bidhaa kwenye mpaka wa Ireland mbili. Ukaguzi huo ni sehemu ya masharti ya kile kinachofahamika kuwa itifaki ya Ireland Kaksazini iliyofikiwa wakati wa mchakato wa Brexit.

Itifaki hiyo italazimisha kuwepo udhibiti mkali wa biashara kati ya Ireland iliyo mwanachama wa Umoja wa Ulaya na Ireland Kaskazini iliyo sehemu ya Uingereza ambayo iliyojotoa Umoja wa Umoja mwaka 2020.