1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme Charles lll kuendeleza amani ya Ireland Kaskazni

Zainab Aziz Mhariri: Yusuf Saumu
13 Septemba 2022

Mfalme Charles wa tatu leo amefanya ziara yake ya kwanza Ireland Kaskazini kama mfalme, akizuru sehemu zote nne za Uingereza kabla ya kufanyika mazishi ya kitaifa ya mama yake Malkia Elizabeth wa pili hapo wiki ijayo.

https://p.dw.com/p/4GnR3
König Charles | Überraschende Fakten | Tee
Picha: Jane Barlow/empics/picture alliance

Mfalme Charles wa tatu baada ya kuwasili Ireland Kaskazini amekaribishwa kwa shangwe na umati wa watu waliokusanyika katika taifa hilo llilogawika juu ya utawala wa kifalme wa Uingereza. Mamia ya watu walijipanga barabarani kuelekea kwenye kasri ya Hillsborough, iliyo nje kidogo ya mji mkuu Belfast ambayo ni makazi rasmi ya familia ya kifalme katika  Ireland ya Kaskazini.

Mfalme Charles lll, Binti Mfalme Anne, Mwana Mfalme Andrew na mManamfalme Edward.
Mfalme Charles lll, Binti Mfalme Anne, Mwana Mfalme Andrew na mManamfalme Edward.Picha: Kai Pfaffenbach/REUTERS

Ingawa makaribisho ni mazuri huko Hillsborough, utawala wa kifalme wa Uingereza huvuta hisia mseto katika Ireland ya Kaskazini, ambako kuna jamuiya mbili kuu: wapo raia wengi wa nchi hiyo wanaoshiriki katika umoja wa Kiprotestanti na ambao wanajiona kuwa ni Waingereza na vilevile wapo waumini wa Kikatoliki wa kanisa la Roma wanaojiona kuwa wao ni  Waairish. Mgawanyiko huo ulichochea ghasia kwa kipindi cha miongo mitatu kati ya makundi ya wanamgambo wa pande zote mbili na vikosi vya usalama vya Uingereza ambapo watu 3,600 walikufa.

Soma Zaidi: Mwili wa Malkia Elizabeth kupelekwa London

Wakati huo huo polisi wa Uingereza wamekosolewa na makundi ya kutetea haki na uhuru wa kijamii kuhusu jinsi wanavyowatendea waandamanaji wanaopinga utawala wa kifalme.

Kwingineko mamia ya watu waliupanga foleni kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Malkia Elizabeth wa pili hadi usiku wa manane wa kuamkia leo nje ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Giles katika mji wa Edinburgh, walipohudhuria mkesha wa kumuaga marehemu Malkia Elizabeth II.

Muonekano wa kasri ya  Buckingham baada ya Malkia Elizabeti ll kufariki.
Muonekano wa kasri ya Buckingham baada ya Malkia Elizabeti ll kufariki.Picha: Maja Smiejkowska/REUTERS

Mfalme Charles wa tatu mwenyewe ameahidi kufuata nyayo za marehemu mama yake, Malkia Elizabeth wa pili kwa kuendeleza msingi wa amani katika Ireland ya Kaskazini. Alizungumza hay oleo Jumanne alipokutana na viongozi wa kisiasa wa Ireland Kaskazini, ikiwa ni pamoja na wale kutoka kwenye vyama vya kitaifa vinvyotaka Ireland Kaskazini ijiondoe kutoka Uingereza na kuwa sehemu ya Jamhuri ya Ireland.

Vyanzo:AFP/AP