1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yatinga robo fainali baada ya kuipiga Ubelgiji 2-1

15 Julai 2022

Ufaransa imejihakikisha nafasi katika robo fainali ya Euro 2022 kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Ubelgiji katika kundi D, katika mechi iliyosaidia kuvunja rekodi ya uhudhuriaji mkubwa zaidi wa michuano hiyo katika historia.

https://p.dw.com/p/4EA7g
Frauen Fußball EM 2022 | Frankreich v Belgien
Picha: Alex Pantling/Getty Images

Kikosi hicho cha Corinne Diacre kilianza vyema kwa goli la kichwa lililofungwa na Kadidiatou Diani kutokana na krosi ya Sakina Karchaoui katika dakika ya sita ya mchezo huo.

Janice Cayman aliifungua Ubelgiji bao la kusawazisha katika dakika ya 36 kwenye uwanja wa New York mjini Rotherham. Lakini Ufaransa, ambao waliigazara Italia kwa mabao 5-1 katika mechi yao ya ufunguzi, walifufuka kutokana na mshtuko huo dakika tano baadae.

Soma pia: Euro 2022: Timu ya wanawake ya Ujerumani yaiadhibu Uhispania 2-0 na kutinga robo fainali

Griedge Mbock Bathy alifunga bao la pili kw akichwa safi akiunganisha krosi kutoka kwa Clara Mateo, na kuhakikisha timu yake inajiunga na sherehe za siku ya Bastille.

Ufaransa, ambayo ilisajili mikwaju 27 dhidi ya miwili ya Ubelgiji, ilipoteza nafasi ya ushindi mkubwa baada ya mchezaji wa Ubelgiji Amber Tysiak kuthibitishwa na teknolojia ya VAR kwamba aliunawa mpira kwenye eneo la boksi.

Frauen Fußball EM 2022 | Frankreich v Belgien
Mfaransa Kadidiatou Diani akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza la timu yake dhidi ya Ubelgiji katika mechi ya kundi D, Julai 14, 2022 mjini Rotherham, England.Picha: Alex Pantling/Getty Images

Makosa ya Tysiak yalipelekea kutolewa nje kwa kuonyeshwa kadi ya pili ya njano, lakini mkwaju wa penati uliopigwa na Wendy Renard uliokolewa na mlinda mlango wa Ubelgiji Nick Evrad. Kocha wa Ufaransa Corrine Diacre, amesema kikosi hakikuwa kizuri kama ilivyokuwa kwenye mechi dhidi ya Italia, huku pia akielezea wasiwasi kuhusu mchezaji wake aliejeruhiwa Marie-Antoinette Katoto.

"Ningeweza kukuambia hata kabla ya mechi kwamba ingekuwa hadithi tofauti. Mechi huja mara chache kwa njia sawa moja baada ya nyingine, na ningesema kamwe haitokei.

Soma pia: Euro 2022: Uholanzi na Sweden zatoka sare

Usiku wa leo tulikosa kidogo uwezo wa kufanya tulioyafanya dhidi ya Italia, lakini bado tumeweza kufunga bao moja zaidi ya wapinzani wetu, na hii ilituwezesha kushinda mechi na kundi," alisema Kocha Diacre.

Ufaransa imeshinda  mechi zao 16 za mwisho katika mashindano yote, wakifunga magoli 69 na kufungwa mara saba tu. Wamewahi kuwa na ushindi mrefu mara tu katika historia yao, wa mechi 17 kati ya Agosti 2011 na Julai 2012.

Frauen Fußball EM 2022 | Frankreich v Belgien
Wachezaji wa Ubelgiji wakisherehekea bao lao la kusawazisha lililofungw akatika dakika ya 36.Picha: OLI SCARFF/AFP

Katika robo fainali, Ufaransa itacheza dhidi ya mshindi wa pili katika kundi C, ambalo kwa sasa linaongozwa na Uholanzi na Swedena ikiwa katika nafasi ya pili.

Soma pia: Euro 2022: England wapata ushindi mwembamba dhidi ya Austria

Ubelgiji wako katika nafasi ya tatu kwenye kundi D, wakiwa na alama moja kutoka michezo mwili. Watalaazimika kuipiga Itali katika mechi yao ya mwisho siku ya Jumatatu ili kuwa na nafasi ya kuipiku Iceland inayoshikilia nafasi ya pili kwa sasa, walio na alama moja mbele yao baada ya kutoka sare ya 1-1 na Italia mapema Alhamisi.

Mechi ya mwisho ya Iceland itakuwa dhidi ya Ufaransa siku ya Jumatatu.

Kocha wa Ubelgiji Ives Serneels, amesema walifanya kila walichoweza kupata matokeo, na anajivunia timu yake licha ya kwamba hawakufanikiwa.

Chanzo. Mashirika