1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUfaransa

Ufaransa kupiga marufuku vazi la Abaya katika shule za umma

28 Agosti 2023

Waziri wa elimu wa Ufaransa Gabriel Attal amesema mamlaka itapiga marufuku wanafunzi kuvaa abaya wakati wanapokuwa shule.

https://p.dw.com/p/4VdGb
Mwanamke wa kiislamu aliyevaa niqab nchini Uswisi
Mwanamke wa kiislamu aliyevaa niqab nchini UswisiPicha: FABRICE COFFRINI/AFP/Getty Images

Vazi la abaya ambalo linachukuliwa kuwa buibui la mtindo wa kisasa huvaliwa na baadhi ya wanawake wa kiislamu kama stara.

Katika mahojiano na shirika la habari la Ufaransa la TF1, waziri huyo ameeleza kuwa atafanya mazungumzo mapema wiki hii na wakuu wa shule za umma ili kuwasaidia kutekeleza marufuku hiyo.

Marufuku hiyo inatarajiwa kuanza kutekelezwa pindi tu muhula mpya wa shule utakapoanza mnamo Jumatatu ijayo.

Ufaransa imepiga marufuku mavazi au alama zozote za kidini katika shule za umma ikisema inafanya hivyo ili kutenganisha serikali na dini.

Inakadiriwa kuwa, waislamu kati ya milioni 3.5 hadi milioni 6 wanaishi nchini Ufaransa, taifa lenye idadi ya watu wapatao milioni 67.