1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Ufaransa, Ujerumani zatangaza mpango wa amani Mashariki

23 Januari 2024

Viongozi wakuu kutoka Ujerumani na Ufaransa wanataka kuimarisha uvumilivu barani Ulaya pamoja na amani na ushirikiano na Mashariki ya Kati kwa kuwa na mradi wa pamoja.

https://p.dw.com/p/4ba6c
Hamburg | Emmanuel Macron und Olaf Scholz
Picha: IMAGO

Kamati ya kupambana na "chuki dhidi ya Wayahudi na chuki dhidi ya wageni barani Ulaya na kuimarisha amani na muingiliano wa kikanda katika Mashariki ya Kati" itaongozwa na aliyekuwa waziri kiongozi wa jimbo la North Rhine Westphalia na mbunge wa Bunge la Ujerumani, Bundestag Armin Laschet pamoja na Leah Pisar na Joel Herzog waliokuwa katika mradi wa Aladdin, wa Ufaransa unaolenga kuimarisha majadiliano kati ya Waislamu na Wayahudi. 

Soma pia: Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Ulaya wataka taifa la Palestina

Laschet na Pisar walitangaza hilo mjini Berlin hapo jana katika maadhimisho ya uhusiano mwema kati ya Ufaransa na Ujerumani. Laschet ni mwenyekiti wa taasisi ya kuimarisha mkataba wa Abraham wa amani na muingiliano wa kikanda.