1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Ulaya wataka taifa la Palestina

22 Januari 2024

Mawaziri wa mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya wamesisitiza hii leo kwamba njia pekee ya kupata amani ya Mashariki ya Kati ni kuanzisha Taifa la Palestina licha ya pingamizi la Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.

https://p.dw.com/p/4bYMc
Umoja wa Ulaya, Israel, Palestina
Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa Umoja wa Ulaya.Picha: Frederic Sierakowski/European Union

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Stephane Sejourne amewaambia waandishi wa habari kwamba maazimio ya Netanyahu yanatia wasiwasi na kuna umuhimu wa Taifa la Palestina kuhakikishiwa usalama.

Ubelgiji, ambayo ni rais wa sasa wa Umoja huo, kupitia Waziri wake Hadja Lahbib, imesema hali katika Ukanda wa Gaza ni ya dharura kutokana na kitisho cha njaa na majanga na kutaka mapigano kusitishwa pamoja na mateka kuachiliwa huru. 

Mawaziri hao wanakutana mjini Brussels kujadiliana mzozo wa Gaza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Israel Katz, pia anahudhuria.