1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa na China zajadili silaha za nyuklia Ukraine

6 Aprili 2023

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akiwa ziarani mjini Beijing amesema kuwa China na Ufaransa zimejadiliana kuhusu vita nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4PnFe
Frankreichs Präsident Macron besucht China - von der Leyen
Picha: Ludovic Marin/Pool AFP/AP/dpa/picture alliance

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akiwa ziarani mjini Beijing amesema leo kuwa China na Ufaransa zimejadiliana kuhusu vita nchini Ukraine na viongozi wa mataifa hayo mawili wameafikiana kuwa silaha za nyuklia hazipaswi kutumiwa katika mzozo huo.

Macron amesema bara la Ulayahaliwezi kuwa salama ikiwa Ukraine itaendelea kukaliwa kimabavu na Urusi jambo alilosema halikubaliki na kuwa Moscow inakiuka mikataba ya Umoja wa Mataifa.

Kwa upande wake, Urusi imesema haina matarajio kuwa China itakuwa mpatanishi katika mzozo wa Ukraine na kwamba haina njia nyingine zaidi ya kuendelea na mashambulizi yake.

China ambayo haijaegemea upande wowote katika mzozo huo, imekuwa ikitoa pendekezo la makubaliano ya amani ambayo yamekuwa pia yakitupiliwa mbali na Marekani.