1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika Kusini

Uchunguzi wa maafa ya moto waanza Afrika Kusini

26 Oktoba 2023

Kumeanzishwa kikao cha uchunguzi leo kilicho na lengo la kubaini aliyehusika na mkasa wa moto huko Johannesburg nchini Afrika Kusini uliosababisha vifo vya watu 77.

https://p.dw.com/p/4Y4PZ
Jengo lililoungu na kusababisha vifo vya watu 77 Johannesburg
Jengo lililoungu na kusababisha vifo vya watu 77 JohannesburgPicha: Michele Spatari/AFP/Getty Images

Uchunguzi huo unayamulika magenge yanayoyateka majengo yaliyotelekezwa mjini humo na kuyakodisha kinyume na sheria. Katika mojawapo ya mikasa mibaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya mji wa Johannesburg, moto huo ulizuka mnamo Agosti 31 katika jengo la zamani lililokuwa limejaa wahamiaji.

Sehemu kubwa ya wahanga waliteketea kiasi cha kutotambulika. Wakati wa tukio hilo, wakaazi wa eneo hilo walisema kwamba jengo hilo lilikuwa limechukuliwa na magenge ya uhalifu.

Johannesburg ni mojawapo ya miji iliyo na pengo kubwa kati ya maskini na matajiri huku umaskini wa kiúpindukia, ukosefu wa ajira na uhaba wa muda mrefu wa nyumba yakiwa baadhi ya matatizo yanayoukabili mji huo.