1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa Zimbabwe: Raia wajiandaa kupiga kura

29 Julai 2018

Watu wa Zimbabwe watapiga kura Jumatatu ya kumchagua rais wa nchi hiyo, kwa mara ya kwanza tangu kumalizika enzi ya Robert Mugabe.

https://p.dw.com/p/32GkS
Simbabwe Wahlen
Picha: DW/C. Mavhunga

Kwa muda wa miaka mingi walichosikia watu kutoka Zimbabwe ni habari juu ya udikteta, mauaji na mgogoro mkubwa wa uchumi. Watu wengi nchini Zimbabwe wanalalamika juu ya maisha yao. Mchuuzi mmoja TinasheLewy amesema maisha ni magumu.Uchumi wa Zibambwe ulianguka wakati wa utawala wa Robert Mugabe.

Mfumuko wa bei ulifikia asilimia milioni 231. Sarafu ya Zimbabwe ilitelekezwa. Sarafu inayotumika zaidi nchini humo sasa ni dola ya Marekani ama watu wananunua vitu kwa hati.Malipo yanafanyika  kwa njia ya benki kutokana na matumizi ya hati hizo .Hali inakuwa ngumu kwa mfanyabiashra mdogo kama Tinashe Lewy kwa sababu hakuna anaeruhusiwa kutoa benki zaidi ya dola 60 kwa wiki.Utaratibu huo huwalazimsisha wafanya biashara kubadilisha hati zao za fedha kwa njia ya magendo na hivyo kuingia hasara kutokana na kubadilisha hati hizo chini ya thamani yake. 

Robert Mugabe aliondolewa kwa nguvu kutoka madarakani mnamo mwezi wa Novemba mwaka uliopita. Jeshi ndio lilimwondoa na mahala pake tangu wakati huo pameshikwa na makamu wake Emmerson Mnangagwa ambae pia alikuwa mshirika wake mkuu. Mnangagwa amesema nataka kuleta mabadiliko. Katika ziara zake za nje Mnangagwa anafanya kampeni ya kuitisha vitega uchumi.

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe
Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert MugabePicha: Reuters/S. Sibeko

Tangu aingie madarakani uwepo wa majeshi ya usalama umepungua hadharani. Mnangagwa pia anajaribu kushikamana na wakulima wa kizungu walionyang'anywa mashamba yao katika enzi za Mugabe. Rais huyo wa Zimbabwe amasema watu wanapaswa kujenga tabia inayokubali kwamba watu wa Zimbabwe ni wamoja.

Hata hivyo chama cha rais Mnangagwa cha ZANU PF hakina mpango wa kuachana na sehemu fulani ya historia yake. Mnamo mwezi juni aliponea chuchupu baada ya bomu kulipuka kwenye mkutano wa hadhara ambako alikuwa anafanya kampeni ya uchaguzi. Mnangagwa alidai kwamba shambulio hilo lilifanywa na washirika wa mke wa Mugabe. Hata hivyo watu wengi wanatilia mashaka madai ya Mnangagwa.

Mkuu wa ofisi ya wakfu wa Adenauer mjini Harare David Mbae amesema ni vigumu kuamini iwapo watu wa serikali hiyo hiyo iliyosababisha uchumi uanguke, waliojitajirisha wenyewe na kubana haki za wananchi  sasa ghafla tu, watu hao ndio walete mageuzi.

Kiongozi muhimu wa upinzani Nelson Chamisa pia haamini iwapo mabadiliko ya kweli yataletwa na watu hao hao wa ZANU PF. Kiongozi huyo wa upinzani mwenye haiba ya kuvutia anakusudia kujenga viwanda uchumi mzuri nakutenga nafasi za ajira nchini Zimbabwe. Hata hivyo bwana Chamisa hajaeleza vipi ataweza kuyafikia malengo hayo. Chamisa ameahidi kujenga treni ya kisasa ya mwendo kasi. Ametoa ahadi hizo licha ya nchi yake kulemewa na deni kubwa sana la mabilioni. Amewaambia wafuasi wake kwamba Zimbabwe inaweza kuiga mfano wa Marekani na China.

Kiongozi wa chama cha Upinzani cha MDC-T Nelson Chamisa
Kiongozi wa chama cha Upinzani cha MDC-T Nelson ChamisaPicha: DW/P. Musvanhiri

Hata hivyo kwa mara ya kwanza katika historia ya Zimbabwe wafuasi wa chama cha upinzani wameweza kufanya kampeni za uchaguzi nje ya mji mkuu, Harare. Mnamo miaka iliyopita watu hao  walikuwa wanaficha sare za vyama vyao kwa kuhofia kushambuliwa na polisi.

Mjumbe wa Umoja wa Ulaya anayeongoza waangalizi wa uchaguzi kutoka kwenye umoja huo Elmar Brok amesema mpaka sasa hakuna vitendo vya chama tawala kuwatisha wapinzani. Hii ni kwa mara ya kwanza baada ya miaka 16 kwa waangalizi wa uchaguzi kutoka nje kuruhusiwa kuingia Zimbabwe.

Mwandishi: Zainab Aziz/ Kriesch Adrian

Mhariri: Isaac Gamba