TUME YA UCHUNGUZI MAPUTO
24 Machi 2007Matangazo
JOHANNESBERG:
Rais Armando Guebuza wa Msumbiji ameteua Tume ya uchunguzi juu ya miripuko katika ghala za silaha kwenye mitaa ya wakaazi katika kitongoji cha Maputo,mji mkuu.Miripuko hiyo imeua watu 96 na kuwajeruhi 400.
Tume hiyo ya uchunguzi inatazamiwa kuripoti mnamo muda wa majuma mawili.Msumbiji imetangaza siku 3 za maombolezi.