1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tume ya Kutetea haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kumteua mchunguzi maalum kusimamia haki za binadamu Darfur

22 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFKn

Tume ya Umoja wa Mataifa ya kutetea haki za binadamu iimekubali kumteua mchunguzi maalum atakayesimamia haki za binadamu katika eneo la Darfur.

Mchunguzi huyo atahitajika kuripoti jinsi hali ya mambo ilivyo kwa tume hiyo pamoja na baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Hili ni sharti moja wapo la azimio lililopitishwa baada ya majadiliano ya Geneva kati ya mataifa ya Umoja wa Ulaya na Afrika. Azimio hilo linalaani kuenea kwa visa vya ukiukaji wa haki za binadamu katika Darfur. Lakini halitaji kuhusika kwa serikali ya Khartoum kama vile Umoja wa Ulaya ulivyokuwa ukitaka.

Takriban watu zaidi ya laki moja wanakisiwa wameuwawa katika eneo hilo na zaidi ya milioni mbili kuachwa bila maskani kufuatia mashambulizi ya wanamgambo wa kiarabu wanaungwa mkono na serikali ya Khartoum.