1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOULOUSE UFARANSA:´Ndege ya Airbus 380 yaanza safari ya majaribnio

27 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFIs

Ndege kubwa duniani ya abiria itwayo Airbus 380 imeanza safari yake ya majaribio hii leo.

Ndege hiyo imeondoka kutoka uwanja wa ndege wa Toulouse Ufaransa kwa majaribio ya masaa matano angani .

Umati wa watu wanaokisiwa kufikia elfu 50 walitarajiwa kukusanyika katika uwanja huo wa ndege kuangalia ndege hiyo ikiondoka.

Ndege hiyo yenye engine nne imeundwa kuwabeba hadi abiria 840 na kusafiri umbali wa kilomita elfu 16 bila kutuwa.

Baadhi ya sehemu ya ndege hiyo ziliundwa hapa Ujerumani ,Uingereza na spain kabla ya kupelekwa katika uwanja wa Toulause Ufaransa.