1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TORONTO:Watu 309 wanusurika kifo katika ajali ya ndege iliyoteketea moto,Toronto Canada

3 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEoH

Ndege kubwa ya abiria ya shirika la ndege la Ufaransa imepata ajali mapema leo asubuhi na kushika moto wakati ilipokuwa inajaribu kutua kwenye uwanja wa ndege wa Pearson mjini Toronto Canada.

Maafisa katika uwanja wa ndege wamesema watu kumi na nne walijeruhiwa kwenye ajali hiyo.Hata hivyo shirika la ndege hiyo limethibitisha kwamba abiria wote 309 pamoja na wafanyikazi wa ndege hiyo waliokuwemo ndani walinusurika kifo.

Kwa mujibu wa abiria ajali hiyo ilisababishwa na hali mbaya ya hewa .

Lakini taarifa ambazo hazijathibitishwa zinaeleza ndege hiyo iliyokuwa inatoka Paris, Ufaransa ilijaribu kutua lakini ilikwenda kasi na kuuvuka mpaka wa barabara yake kwa umbali wa mita 200 na kusababisha ajali hiyo.