Tofauti 10 kubwa kati ya China na Ujerumani
China na Ujerumani hazina tofauti kubwa sana lakini kuna 10 kubwa zinazoonyesha tofauti za kipekee kati ya mataifa hayo mawili.
Utamaduni wa shule
China ni moja kati ya mataifa machache duniani ambapo wazazi wanaweza kupinga sera ya kazi za ziada za shule kufanyiwa nyumbani. Wanafunzi nchini China wanapaswa kuzowea utaratibu wao wa kiufundi kutoka umri mdogo. Saa za shule ni kutoka saa 7.30 asubuhi hadi saa 9 jioni kwa siku sita na nusu kwa wiki. Maandalizi ya mtihani wa kitaifa yanaaza miaka 7 kabla ya mtihani huo.
Utawala wa familia
Nyumba ya kawaida: vizazi vitatu vinaishi chini ya paa moja. Babu na nyanya wanajukumu la kulea watoto huku wazazi wao walio na shughuli nyingi wakiendeleza taaluma zao. Watoto wanahimizwa kuishi kwa muda mrefu kama wanavyotaka katika nyumba za wazazi wao. Kulazimishwa kuhama nyumbani katika umri wa miaka 18 na kumuita mtu mzima kwa jina lake la kwanza sio jambo la kawaida na hairuhusiwi.
9-9-6
Saa 12,5 kwa siku kwa miaka 12 inaugumu gani iwapo unatarajiwa kufanya kazi kwa saa 12 kwa siku miaka yako yote? Jack Ma, mwanzilishi wa kampuni ya Ali Baba, anapendekeza kufanya kazi kutoka saa tatu asubuhi hadi saa tatu usiku, siku sita kwa wiki. Katika taarifa kwa wafanyikazi wenzake, Ma alisema," munapoteza ujana wenu iwapo hamutatumia mfumo huu wa 996."
Nafasi ya kibnafsi
Mikoa yote 22 nchini China husherehekea sikukuu sawa. Hiyo ni kumaanisha watu bilioni 1 wako huru kutembea kwa wakati mmoja. Katika bwawa moja la kuogelea la umma mjini Fushun, China, siku ya joto huvutia idadi kubwa ya watu katika maji hayo baridi. Iwapo mtu atalalamika kuhusu idadi kubwa ya watu, wakazi wa eneo hilo hujibu, “ Hii ni China, unatarajia nini?
Viwango vya usafi
China imeorodheshwa miongoni mwa mataifa kumi ya kwanza yenye maeneo ya miji yalio na kiwango kikubwa cha uchafuzi duniani. Pia ni moja kati ya mataifa yanayoongoza duniani katika uvutaji wa sigara. Ujumuishaji wa masuala haya unachangia kiwango duni cha hewa safi.
Utegemeaji wa teknologia
Huku kukiwa na mfumo wa simu kwa takriban huduma zote, China inawekeza zaidi katika ukuaji wa teknologia. Washawishi nchini China wanapata mapato ya hadi dola elfu 20 kwa mwezi kutuma habari katika mitandao yao ya kijamii. Kwa mfano: wasafiri wanaoangalia simu zao wanaposafiri kila siku. Wengine wakicheza video, wengine wakisoma vitabu mtandaoni.
Pesa
Wakati mmoja pesa ilikuwa kama mfalme, lakini wakati nambari za siri za simu zilipoanza kutumiwa mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili, mengine yalikuwa historia. Ikizingatiwa kuwa kiwango kikubwa cha dola ya China ni takriban dola 16 za Marekani, malipo kupitia simu yameleta mwamko mpya katika mifumo ya matumizi ya China.
Ulinzi wa habari
“kama sifanyi kitu kibaya, kwanini niwe na wasiwasi?” ndilo jibu kuhusiana na masuala ya ulinzi wa habari. Mfumo wa simu wa kutuma ujumbe wa China -wechat- unatambulika kwa kuzuia maneno machafu katika kuwasiliana. Kiunganishi cha mawasiliano ya mtandaoni cha umma bila malipo, kinahitaji nambari ya simu ya rununu kujisajili na kuidhinishwa kwa matumizi yake kupitia matakwa yao.
Kaka mkubwa anatazama
Mfumo wa sifa kwa umma nchini China unatokana na kutambuliwa kwa sura kupitia kamera za siri zilizoko katika barabara na taa za barabarani kote nchini humo. Kutokana na teknologia hii, kamera zinaweza kumtambua mtu kutokana na maumbile yake na mtindo wa kutembea bila ya hata kuangalia sura. Serikali inapanga kuwa na kamera za siri milioni 570 katika mtandao wake kufikia mwaka 2020.
Mifumo ya sifa kwa umma
Kuhakikisha sheria na utaratibu vinadumishwa katika taifa lenye idadi ya watu bilioni moja sio rahisi. China inahakikisha kuwa raia wake wanazingatia sheria kwa kuwapa alama. Alama hizi hubadilika kutokana na jinsi wanavyojibeba katika maeneo ya umma ama kwa kufuatilia mtindo wao wa matumizi miongoni mwa masuala mengine. Mfumo huu unanuia kuimarisha ukweli.