1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ni Taifa Stars na Morocco Benjamin Mkapa leo

21 Novemba 2023

Timu ya taifa ya Rwanda watakipiga na Bafana Bafana ya Afrika ya kusini saa kumi jioni kwa saa ya Afrika ya mashariki, Timu ya taifa ya Uganda, Uganda the Cranes watakuwa ugenini kucheza na Somalia katika muda huo huo.

https://p.dw.com/p/4ZFiM
Timu ya taifa ya Morocco
Kikosi cha timu ya taifa ya Morocco.Picha: imago images/Sebastian Frej

Mechi za kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia mwaka 2026 huko Marekani, Mexico na Canada zinaendelea hii leo, Timu za mataifa ya Afrika ya Mashariki zinaendelea kutupia karata zao hii leo.

Soma zaidi:FIFA: Michuano ya Kombe la Dunia 2030 kuchezeka katika mabara 3

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo watakuwa nyumbani katika uwanja wa taifa wa Benjamin Willium Mkapa kucheza na timu ya taifa ya Morocco ( Simba wa Atlas), huu utakuwa ni mchezo wa pili kwa timu ya taifa ya Tanzania baada ya ushindi wa goli moja sifuri ugenini dhidi ya Niger huku Morocco wakitupia karata yao ya kwanza. 

Michezo ya kuwania kucheza kombe la dunia .
Wachezaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast na Gambia wakiwa katika heka heka katika mchezo wa kuwania kucheza Kombe la Dunia 2026 katika uwanja wa Benjamin Mkapa- Dar-es-Salaam, Tanzania.Picha: Loveness Bernard/empics/picture alliance

Soma zaidi: Mamelodi Sundowns mabingwa wa kwanza wa michuano ya AFL

Mchezo kati ya Taifa Stars na Simba wa Atlas utachezwa saa nne kamili usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki.

Timu ya taifa ya Rwanda ya Amavubi watakipiga na Bafana Bafana ya Afrika ya kusini saa kumi jioni kwa saa ya Afrika ya mashariki, Timu ya taifa ya Uganda, Uganda the Cranes watakuwa ugenini kucheza na Somalia katika muda huo huo

Sikiliza pia:

Rwanda itatamba mbele ya Bafana Bafana?

Timu ya taifa ya Kenya ya Harambee Stars walicheza usiku wa kuamkia leo na kuwachabaga Usheli Sheli magoli matano kwa mtungi.