1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamelodi Sundowns mabingwa wa kwanza wa michuano ya AFL

Sylvia Mwehozi
13 Novemba 2023

Klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imeshinda taji la kwanza la michuano mipya ya Ligi ya Soka ya Afrika AFL, baada ya kuilaza Wydad Casablanca ya Morocco mabao 2-0.

https://p.dw.com/p/4YjAT
Finali ya Champions League ya CAF
Mamelodi Sundowns wakisherehekea ubingwa wa ligi ya mabingwa mwaka 2016Picha: Ahmed Gamil/AP Photo/picture alliance

Klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imeshinda taji la kwanza la michuano mipya ya Ligi ya Soka ya Afrika AFL, baada ya kuilaza Wydad Casablanca ya Morocco mabao 2-0 katika mechi ya mkondo wa pili. Katika mechi ya kwanza iliyopigwa Casablanca mwishoni mwa juma lililopita , Mamelodi walifungwa bao 2-1.

Soma: CAF: Al Ahly yaifunga Wydad Casablanca

Hii ni mara ya kwanza kwa Mamelodi kuishinda Wydad katika mechi ya mtoano baada ya kupoteza mara mbili, katika nusu fainali na mara moja katika robo fainali ya ligi ya mabingwa ya CAF kutoka mwaka 2017. Michuano hiyo mipya iliyoanzishwa na shirikisho la soka Afrika CAF, ilizishirikisha timu nane zikiwemo Simba ya Tanzania na TP Mazembe ya Kongo.