1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Theluji yaukumba mji wa kusini mwa Ujerumani wa Munich

2 Desemba 2023

Usafiri wa anga kupitika kiwanja cha ndege cha Munich huko kusini mwa Ujerumani unatarajiwa kusitishwa hadi taarifa nyininge itakapotolewa mchana huu kutoka na kuporomoka kwa kiwango kikubwa cha theluji.

https://p.dw.com/p/4Zhfd
Kuanguka kwa theluji kwa athiri usafiri wa anga mjini Munich nchini Ujerumani
Kuanguka kwa theluji kwa athiri usafiri wa anga mjini Munich nchini UjerumaniPicha: Sean Gallup/Getty Images

Hali hiyo inatajwa kuathiri safari za  ndege zaidi ya 150 katika uwanja wa ndege wa jiji hilo, ambao ni wa pili kwa shughuli nyingi nchini humo.

Kadhia ya theluji iliporomoka kusini mwa Ujerumani na haswa Bavaria Ijumaa usiku, na kusababisha usumbufu mkubwa katika Uwanja wa Ndege wa Munich.

Taasisi ya kutoa huduma ya taarifa ya hali ya hewa ya Ujerumani ya DWD ilitabiri theluji ya muda mrefu hadi Jumamosi alasiri katika sehemu kubwa ya Bavaria, ya kiwango cha takriban sentimeta 30 hadi 40  sawa na takriban inchi 12 hadi 15 cha  theluji.