1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAsia

Tetemeko lingine la kipimo cha 4.9 laikumba Afghanistan

9 Oktoba 2023

Tetemeko lingine la ardhi lenye ukubwa wa 4.9 limetikisa magharibi mwa Afghanistan leo Jumatatu huku zaidi ya watu 2000 wakifariki kwenye tetemeko la mwishoni mwa wiki.

https://p.dw.com/p/4XJNB
Watu wakiendelea kufukua vifusi vya majengo Afganistan baada ya tetemeko
Watu wakiendelea kufukua vifusi vya majengo Afganistan baada ya tetemekoPicha: courtesy of TOLOnews

Mitetemeko mipya imethibitishwa na Utafiti wa Jiolojia wa nchini Marekani na pia wakaazi katika eneo hilo la magharibi mwa Afghanistan.

Tetemeko hilo la kipimo cha 6.3la mwishoni mwa juma liliharibu kabisa takriban vijiji 13 katika wilaya ya Zindah Jan katika mkoa wa Herat.

Soma pia;Watu zaidi 2,000 wafa kwa tetemeko la ardhi Afghanistan

Wakaazi wa eneo hilo na waokoaji bado wanaendelea kuondoa miili ya watu waliokufa kwenye vifusi katika eneo la maafa.