1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Iran na Irak kufanya biashara ya mafuta

18 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEtM

Waziri wa mafuta wa Iran, Bijan Namdar Zanganeh, amesema leo kwamba ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Iran kwenda Irak utaanza hivi karibuni. Tangazo hilo limefanywa wakati waziri mku wa Irak, Ibrahim al-Jafaari akimaliza ziara yake rasmi mjini Tehran.

Bomba hilo ambalo linajengwa kufuatia mkataba uliosainiwa miezi kumi iliyopita, linatarajiwa kuanza kutumika katikati ya mwaka ujao. Litauunganisha mji wa Basra kusini mwa Irak na kiwanda cha kusafishia mafuta mjini Abadan nchini Iran.

Bomba hilo litatumiwa kusafirisha mapipa elfu 150 ya mafuta kila siku na lita milioni 50 za bidhaa za mafuta zikiwemo mafuta ya taa na petroli.