SiasaAfghanistan
Taliban yasaini makubaliano ya dola bilioni 6.5 Afghanistan
1 Septemba 2023Matangazo
Makubaliano haya ni makubwa zaidi tangu Taliban iliporejea mamlakani miaka miwili iliyopita.
Mikataba hiyo imetiwa saini kati ya serikali na makampuni ya ndani ambayo mengi yana ushirika na makampuni kigeni kutoka China, Iran na Uturuki. Aidha mikataba hiyo inahusiana na shughuli za kufua chuma, uchimbaji wa madini ya risasi, zinki na dhahabu katika majimbo manne.
Makubaliano hayo yanatajwa kuwa yatasaidia kuupatikana maelfu ya nafasi za kazi na kuimarisha kwa kiasi kikubwa hali ya uchumi nchini Afghanistan. Hata hivyo hakukuwa na taarifa yoyote kuhusiana na makubaliano hayo kutoka wizara ya Madini na Petroli.