1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Taliban yatangaza kuwauwa wanamgambo wawili wa IS

Hawa Bihoga
27 Februari 2023

Vikosi vya usalama vya Taliban vimewauwa wanamgambo wawili wa kundi la dola la Kiislam na kumkamata wa tatu katika shambulio la usiku katika mji mkuu wa Afghanistan Kabul.

https://p.dw.com/p/4O12x
Afghanistan Kabul | PK der Taliban: Sprecher Zabihullah Mujahid: Mullah Mohammad Hasan Akhundzada soll Taliban leiten
Picha: AAMIR QURESHI/AFP/Getty Images

Msemaji wa serikali ya Taliban Zabihullah Mujahid amesema kwamba, operesheni ilioendeshwa na serikali kuu ya Taliban iliwalenga wanamgambo wa Taliban ambao walipanga kufanya mashambulizi katika mji mkuu wa Afhganistan.

Mujahid ameongeza kwamba katika oparesheni hiyo wamekamata risasi pamoja na vifaa vingine vya kijeshi. Kundi la dola la Kiislam bado halijazungumzia chocote kuhusiana na taarifa ya Taliban.

Mlipuko waua watu zaidi ya 20 Afghanistan

Mshirika wa kikanda wa kundi la dola la Kiislam linalojulikana Dola la Kiislam katika jimbo la Khorasan ni mpinzani mkuu wa Taliban.Tangu Taliban ichukue madaraka wanamgambo wameongeza mashambulizi nchini humo.