1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Mlipuko waua watu zaidi ya 20 Afghanistan

11 Januari 2023

Mshambuliaji wa kujitoa muhanga amejilipua karibu na wizara ya mambo ya nje ya Afghanistan na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 20.

https://p.dw.com/p/4M24z
Afghanistan | Explosion vor Außenministerium in Kabul
Picha: Wakil Kohsar/AFP/Getty Images

Picha kutoka eneo la tukio zinaonyesha maiti zikiwa zimezagaa kwenye theluji barabarani nje ya jengo lililo katikati ya mji wa Kabul.

Dereva wa shirika la habari la Ufaransa AFP Jamshed Karimi amesema hafahamu ni watu wangapi waliouliwa au kujeruhiwa katika shambulizi hilo, lakini amemuona mshambuliaji akijilipua.

Msemaji wa polisi Khalid Zardan amethibitisha kutokea kwa mlipuko huo ambao kwa bahati mbaya umesababisha maafa.