1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTaiwan

Taiwan yabaini ndege na manoari za china karibu yake

14 Septemba 2023

Wizara ya ulinzi ya Taiwan imesema imebaini ndege 68 za kivita za China pamoja na manowari za kijeshi 10 karibu na pwani zake katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita.

https://p.dw.com/p/4WKjf
Meli ya kivita ya China katika ujia wa bahari wa Taiwan
Meli ya kivita ya China katika ujia wa bahari wa TaiwanPicha: Mass Communication Specialist 1st Class Andre T. Richard/U.S. Navy via AP/picture alliance

Taarifa zimesema hadi majira ya saa 12.00 za asubuhi ya leo, ndege 40, zinazojumuisha pia droni za kivita zilikuwa zimevuka mstari wa kati wa Ujia wa Taiwan na kuingia katika eneo la anga la kusinimagharibi na kusinimashariki mwa kisiwa hicho kinachojitawala.

Soma pia:China yafanya luteka ya ´onyo´ kuzunguka Taiwan

Taipei hapo awali ilisema kwamba baadhi ya ndege hizo na manowari zilikuwa zikielekea kwenye eneo ambalo halijulikani la Kaskazini mwa Pasifiki kwa ajili ya mazoezi ya pamoja ya baharini na angani.

Mapema wiki hii, Taiwan ilionya kuhusiana na hatua ya China ya kuimarisha shughuli zake zinazoibua kitisho katika kisiwa hicho.