1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yakasirishwa na makamu wa rais Taiwan kutua Marekani

13 Agosti 2023

China imeapa kuchukua hatua madhubuti na za nguvu kuhusiana na ziara ya mwishoni mwa wiki ya Makamu wa Rais wa Taiwan William Lai nchini Marekani ambayo ilisema inaifuatilia kwa karibu.

https://p.dw.com/p/4V70l
New York City Ankunft Taiwan Vize-Präsident William Lai
Picha: TAIWAN PRESIDENTIAL OFFICE/REUTERS

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni amesema katika taarifa kuwa China itachukua hatua za kulinda mamlaka yake na uadilfu wa mipaka.

Soma pia: China yakasirishwa na safari ya makamu wa rais wa Taiwan kupitia Marekani

Imeongeza kuwa inapinga aina yoyote ya mazungumzo rasmi kati ya Marekani na Taiwan, inapinga vikali wanaharakati wanaotaka kujitenga wanaotafuta uhuru wa Taiwan kuingia Marekani chini ya jina jingine na kwa sababu yoyote na inapinga aina yoyote ya mawasiliano kati ya serikali ya Marekani na upande wa Taiwan.

Lai - mgombea mkuu katika uchaguzi wa rais wa Taiwan mwaka ujao -- atatua Marekani wakati akiwa njiani kwenda na kutoka Paraguay, ambako atahudhuria kuapishwa kwa rais mteule Santiago Pena. China inadai kuwa kisiwa cha Taiwan ni sehemu ya himaya yake, na imeapa kukichukua siku moja kwa nguvu kama itahitajika.