1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SYDNEY:Njama ya mashambulio yazuiliwa Australia

8 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEKb

Polisi nchini Australia wamedai kuwa wamezuia shambulio kubwa la kigaidi kwa kuwakamata washukiwa 6 mjini Sydney na wengine 9 katika mji wa Melbourne.Washukiwa hao wanafikishwa mahakamani leo Jumanne.Miongoni mwa mashtaka ni uanachama wao katika kundi lililopigwa marufuku.Polisi hawakueleza mashambulio hayo yalilenga vituo gani,lakini walisema kuwa matayarisho ya mashambulio hayo yalikuwa katika hatua za mwisho na kemikali zilizokutikana,labda zilikuwa kwa ajili ya kutengenezea mabomu. Washukiwa hao wamekamatwa siku chache tu baada ya serikali kufanya mageuzi ya sheria za kupiga vita ugaidi,ili kurahisisha kuwakamata watuhumiwa.Vyama vya upinzani viliituhumu serikali kuwa inawatisha raia.