1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUswidi

Sweden yavuka kihunzi kingine uanachama wa Jumuiya ya NATO

27 Desemba 2023

Kamati ya Mambo ya Kigeni ya Bunge la Uturuki imeridhia maombi ya Sweden kujiunga na Jumuiya ya Kujihami ya NATO, uamuzi unaoongeza matumaini kwa taifa hilo kukaribia kuwa mwanachama kamili wa mfangamano huo wa kijeshi.

https://p.dw.com/p/4abF1
NATO
Viongozi wa Uturuki (kushoto) na Sweden (kulia) walipokutana mkutano wa NATO uliofanyika mapema mwaka huu mjini Vilniua, Lithuania.Picha: Henrik Montgomery/ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Itifaki ya maombi ya uanachama wa Sweden sasa itasubiri kuidhinishwa na bunge zima la Uturuki ikiwa ni hatua ya mwisho kwa mchakato huo. Bado hakuna tarehe rasmi iliyopangwa kwa ajili ya kura hiyo.

Uturuki, moja ya mataifa 31 wanachama wa NATO, imechelewesha kwa karibu mwaka mmoja maombi ya kujiunga kwa Sweden baada ya kuituhumu nchi hiyo kutochukua hatua stahiki dhidi ya makundi yanayotishia usalama wa Uturuki.

Miongoni mwa makundi hayo ni ya wanamgambo wa Kikurdi na mtandao wa wafuasi wengine wa upinzani unaoshukuwa kuwa sehemu ya jaribio la mapinduzi la mnamo mwaka 2016 nchini Uturuki.