1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaItaly

Viongozi wakuu wa G7 wajadili uhamiaji

14 Juni 2024

Viongozi wakuu wa mataifa ya G7 wameelekeza mawazo yao katika suala la uhamiaji, kutafuta njia za kupambana na biashara haramu na kuongeza uwekezaji katika nchi wanakotokea wahamiaji.

https://p.dw.com/p/4h3NB
Italia | Wakuu wa G7 wakimpongeza Kansela wa Ujerumani katika siku yake ya kuzaliwa
Wakuu wa mataifa ya kundi la G7 katika mkutano wao uliofanyika nchini ItaliaPicha: Steffen Kugler/BPA/dts Nachrichtenagentur/IMAGO

Miongoni mwa mengi yaliyojadiliwa katika mkutano huo, ni pamoja na msaada zaidi kwa Ukraine, vita vya Gaza, teknolojia ya akili mnemba, mabadiliko ya hali ya hewa na uwezo wa kiviwanda wa China uliopitiliza.

Hata hivyo kumeibuka migawanyiko kabla ya tamko rasmi la mkutano huo, kuhusu kutokubaliana juu ya kujumuishwa kwa mada ya uavyaji mimba.

Akizungumza katika mkutano Kiongozi  mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis  ametoa wito wa kupigwa marufuku kwa silaha hatari zinazojiendesha za akili mnemba.