1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan yatimiza siku 100 za mapigano

24 Julai 2023

Miripuko imeendelea kuripotiwa kutokea katika maeneo tofauti ya Sudan ikiwa taifa hilo jana Jumapili likitimiza siku 100 za mapigano

https://p.dw.com/p/4UJI2
Südsudan Rubkona County | Flüchtlinge
Picha: Isaac Mugabi/DW

Siku hizo 100 zinatimizwa katika kipindi ambacho timu za wapatanishi za kikanda na kimataifa zikionekana kushindwa kudhibiti hali inayoongezeka kuwa mgumu zaidi.

Mapigano yalianza Aprili 15 pale ambapo jeshi na kikosi chake cha kukabiliana na matukio ya dharura cha RSF kuingia katika mzozo wa kuwania madaraka. Tangu wakati huo zaidi ya watu milioni 3 wamevurugiwa makazi yao, wakiwemo zaidi ya 700,000 ambao wamekimbilia mataifa ya jirani na Sudan. Kwa mujibu wa wizara ya afya ya taifa hilo watu 1,136 wameuwawa, ingawa maafisa wenyewe wanasema idadi kamili kimsingi inaweza kuwa kubwa zaidi ya hiyo inayoainishwa.

Maisha ya magumu ya Wasudan kambini Chad

Tschad Geflüchtete Sudan Flüchtlingslager von Toumtouma
Hali ya Wakimbizi wa Sudan nchini Chad bado inaelezwa kutokuwa nzuriPicha: Blaise Dariustone/DW

Akiwa katika kambi ya Andre, nchini Chad, Zainab Abdallah analezea hali ngumu waliyopitia wakiwa Sudan na ilivyo sasa huko Chad."Walichoma nyumba zetu na kuua watu. Nyumba yangu imechomwa, na sina nyumba sasa, na sina la kufanya. Ninajenga nyumba kwa kutimia miti, majani ya miwa na nailoni, lakini Mungu ni mwenye neema.”

Hadi wakati huu, si jeshi wala RSF walioweza kijitangazia ushindi katika vita hivyo,pamoja na kwamba RSF inaonekana kuwa na nguvu katika maeneo ya mji mkuu wa Khartoum ikikabaliana na mashambulizi ya anga na makombora mengine ya mizinga kutoka kwa jeshi la nchi hiyo.

Miundombinu na serikali katika mji mkuu vimevurugika katika kipindi ambacho mapigano yanatajwa kusambaa hadi huko magharibi, haswa hadi eneo tete la Darfur, na pia kusini, ambapo waasi Kundi la SPLM-N limejaribu kudhibiti eneo hilo.

Mapigano yanaendelea Sudan na watu 20 wameuwawa.

Mwishoni mwa wiki, kundi la RSF lilionekana kuingia katika maeneo ya vijiji vya Gezira, Jimbo lililo upande wa kusini mwa Khartoum, ambapo jeshi lilifanya mashambulizi ya anga dhidi yao. Taarifa hiyo ni kwa mujibu ya walioshuhudia.

Kwa mujibu ya walioshuhudia pia kwa upande wa kusini mwa Darfur, mji mkubwa wa Nyala mapigano yamekuwa yakiripotiwa katika maeneo ya makazi ya watu tangu Alhamis iliyopita. Vyanzo vya watoa tiba vinasema watu 20 wameuwawa. Na Umoja wa Mataifa unasema familia 5,000 zimeachwa bila ya makazi, kadhalika wakazi wametoa ripoti ya vitendo vya uporwaji wa vifaa muhimu.

Katika maeneo hayo, Salah Abdallah mwenye umri wa miaka 35 anasema risasi zimekuwa zikivurumishiwa katika makazi yao na kwamba pamoja na hofu waliyonayo lakini pia hakuna yeyote mwenye kuonesha nia ya kutaka kuwalinda.

Soma zaidi:Mashambulizi ya makombora yasababisha vifo vya watu 20 Sudan

Lakini pia JumaMashambulizi ya makombora yasababisha vifo vya watu 20 Sudanpili jioni, jeshi la Sudan limesema watu tisa wamekufa wakiwemo wanajeshi wake wanne baada ya ndege ndogo ya abiria kuanguka kutokana na hitilafu huko katika uwanja wa ndege wa Port Sudan, mashariki mwa taifa hilo. Taarifa hiyo iliongeza kuwa binti mdogo wa kike alinusurukia katika ajali hiyo.

Chanzo: RTR