1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya makombora yasababisha vifo vya watu 20 Sudan

23 Julai 2023

Takribani raia 20 wa Sudan wameuawa katika mashambulizi ya makombora yaliyorushwa katika maeneo ya makaazi ya mojawapo ya miji muhimu ya Darfur na karibu na hospitali katika jimbo la Kordofan Kaskazini.

https://p.dw.com/p/4UHWD
Wanajeshi wa Sudan wakiwa Darfur
Wanajeshi wa Sudan wakiwa DarfurPicha: Ashraf Shazly/AFP/Getty Images

Chama cha Madaktari kilisema kwamba tangu mapema siku ya Ijumaa, makombora yalirushwa karibu na hopsitali nne katika mji mkuu wa jimbo la Kordofan Kaskazini na kuwaua raia wanne na wengine 45 walijeruhiwa.

Soma zaidi: Machafuko yaibuka tena katika mji mkuu wa Sudan

Katika mji mkuu wa jimbo la Darfur wa Nyala, chama cha wanasheria kimethibitisha vifo vya watu 16 vilivyosababishwa na shambulio la kombora.

Mkoa wa Darfur ambao tayari umegubikwa na mzozo mbaya katika miaka ya 2000, umeshuhudia ghasia mbaya tangu mapigano yalipozuka katikati ya mwezi wa nne baina ya Majenerali hasimu wa Sudan wanaowania madaraka.