1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Sudan yasitisha mahusiano na IGAD kufuatia mwaliko wa Daglo

17 Januari 2024

Sudan imetangaza kusitisha mahusiano na Jumuiya ya IGAD kwa uamuzi wake wa kumwalika kiongozi wa kikosi cha wanamgambo wanaopigana na jeshi la taifa, kwenye mkutano wa kilele utakaofanyika baadaye wiki hii.

https://p.dw.com/p/4bLTa
Mkutano wa IGAD | Addis Abbaba
Jumuiya ya IGAD imekuwa mstari wa mbele kutafuta suluhu ya mzozo wa SudanPicha: Office of the PM Ethiopia

Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya kigeni ya Sudan, imesema uamuzi wa IGAD wa kumkaribisha kiongozi wa kikosi cha RSF, Mohammed Hamdan Daglo, kuhudhuria mkutano wa kilele wa jumuiya hiyo utakaofanyika kesho Alhamisi ni "ukiukaji mkubwa wa hadhi na uhuru" wa taifa hilo.

Hadi sasa Jumuiya hiyo haijatoa majibu yoyote kuhusu tuhuma hizo wala kuthibitisha mwaliko wa Daglo kwenye mkutano huo wa kilele wa 42 utakaofanyika mjini Kampala nchini Uganda.

Jumuiya ya IGAD yenye mataifa nane wanachama imekuwa ikiongoza juhudi za kikanda kuutafutia suluhu mzozo wa Sudan uliozuka April mwaka jana.