1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Sudan yakataa usuluhushi wa Afrika Mashariki

14 Januari 2024

Serikali inayoungwa mkono na jeshi la Sudan imepuuzia mbali mwaliko wa kuhudhuria mkutano wa kilele wa Afrika Mashariki na imeukemea Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na kamanda wa vikosi hasimu.

https://p.dw.com/p/4bDdu

Miezi tisa baada ya vita kuzuka kati ya jeshi kuu na vikosi vya vya msaada wa haraka jeshi hilo kuu limekuwa likipoteza maeneo, wakati ambapo kiongozi wa vikosi vya dharura Mohamed Hamdan Dagloamekuwa akizuru miji mikuu ya Afrika ili kujenga hadhi ya kidiplomasia.

Kiongozi wa baraza la mpito la nchini Sudan, jenerali Abdel Fattah al Burhan amekataa mwaliko wa kuhudhuria mkutano wa nchini Uganda, tarehe 18 mwezi huu kwa sababu nchi za Afrika Mashariki, za jumuiya ya IGAD pia zimemwalika hasimu wake, Mohamed Hamdan Daglo ambaye ni kiongozi wa kikosi kilichoasi cha RSF.

Jumuiya ya IGAD mara kwa mara imejaribu kuwapatanisha mahasimu hao wawili lakini juhudi hizo zinapingwa na serikali ya jenerali Burhan.