1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan yakataa kushiriki mkutano wa IGAD na Kenya

11 Julai 2023

Serikali inayoongozwa na jeshi nchini Sudan imekataa kushiriki mazungumzo ya kusaka amani yaliyoitishwa na Jumuiya ya Ushirikiano wa Pembe ya Afrika (IGAD) ikiituhumu Kenya kuliunga mkono kundi la wanamgambo wa RSF.

https://p.dw.com/p/4TiXl
Äthiopien | IGAD Treffen in Addis Ababa | William Ruto und Abiy Ahmed Ali
Picha: State House of Kenya/AA/picture alliance

Serikali ya Sudan imekataa kushiriki katika mkutano wa kikanda unaolenga kumaliza karibu miezi mitatu ya mapigano ya kikatili, ikiishutumu Kenya, ambayo ilikuwa mwenyekiti wa mazungumzo hayo, kwa kuwapendelea wanamgambo hasimu wa RSF.

Soma zaidi: Mapigano makali kati ya majenerali hasimu yaendelea Sudan

Jumuiya ya nchi za Mashariki na Pembe ya Afrika (IGAD) ilizialika pande mbili hasimu kwenye mkutano uliofanyika katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, siku ya Jumatatu (Julai 10) wakati mapigano yakiendelea kote nchini Sudan.

Mkuu wa Majeshi wa Sudan, Jenerali Abdul-Fattah Al-Burhan na mkuu wa kundi la wanamgambo wa RSF, Mohamed Hamdan Daaglo, hawakuhudhuria moja kwa moja mazungumzo hayo, ingawa kundi la RSF lilituma mwakilishi kwenye mkutano huo ulioongozwa na Kenya, Sudan Kusini, Djibouti na Ethiopia.

Soma zaidi: Mapigano ya Sudan yaingia siku ya sita na kuua watu 300

Wizara ya mambo ya nje ya Sudan ilisema katika taarifa kuwa ujumbe wake isingelishiriki hadi ombi lake la kuiondoa Kenya kama mwenyekiti wa mazungumzo hayo litimizwe.

"Tunataka Rais William Ruto wa Kenya abadilishwe kwa sababu ya upendeleo wake." Ilisema taarifa hiyo.