1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

STRASBOURG. Mahakama ya haki za binadamu yatupilia mbali kesi.

30 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFRx

Mahakama ya haki za binadamu ya Ulaya imetupilia mbali malalamiko ya Wajerumani wa liokuwa wakiishi Ujerumani Mashariki kuhusu ardhi yao walionyang’anywa baada ya mwaka 1945.

Wajerumani sabini na moja kutoka Mashariki ya Ujerumani walitaka kupitia mahakama ya Strasbourg walipwe fidia kufuatia kuchukuliwa kwa ardhi na majeshi ya Sovieti baada vita vya pili vya ulimwengu.

Mahakama ya Strasbourg imeunga mkono uamuzi wa mahakama ya Ujerumani dhidi ya malalamiko hayo jambo ambalo linaiepushia serikali ya Ujerumani kulipa fidia ya mabilioni ya Euro.