1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Stoltenberg aelezea matumaini ya Sweden kujiunga na NATO

23 Februari 2023

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami NATO, Jens Stoltenberg amesema leo kuwa ameona maendeleo katika mzungumzo na Uturuki kuhusu maombi ya uanachama ya Sweden

https://p.dw.com/p/4NtiS
Belgien | NATO | Treffen Jens Stoltenberg mit Dmytro Kuleba und Josep Borrell
Picha: Valeria Mongelli/AFP/Getty Images

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami NATO, Jens Stoltenberg amesema leo kuwa ameona maendeleo katika mzungumzo na Uturuki kuhusu maombi ya uanachama ya Sweden, na ananuwia kuwa Sweden na Finland zinajiunga na muungano huo wakati wa mkutano wake wa kilele utakaofanyika mwezi Julai.

Soma pia: Biden akutana na viongozi wa NATO wa mashariki mwa Ulaya

Stoltenberg ameliambia shirika la habari la Reuter kwamba yeye na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wamekubaliana kwamba Uturuki, Finland an Sweden zitakutana makao makuu ya NATO katikati mwa mwezi Machi kuzungumzia changamoto zinajitokeza linapokuja suala la Uturuki kuridhia uanachama wa Sweden.

Sweden na Finland ziliomba kujiunga na NATO mwaka jana, baada ya Urusi kuivamia Ukraine, lakini Sweden ilikabiliwa na upinzani usiotarajiwa kutoka Uturuki.

Ankara inaishtumu Stockholm kwa kuwahifadhi watu ambao Uturuki inawachukulia kuwa wanachama wa makundi ya kigaidi, na ilitaka wakabidhiwe kwake, kama sharti la kuridhia maombi yake.