1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO:Wakati wa kuridhia Finland na Sweden kujiunga

16 Februari 2023

Katibu mkuu wa jumuiya ya kujihami ya NATO Jens Stoltenberg amesema huu ni wakati muafaka wa Uturuki kuridhia maombi ya Finland na Sweden ya kujiunga na muungano huo wa kijeshi.

https://p.dw.com/p/4Nbe2
Türkei NATO Mevlut Cavusoglu Jens Stoltenberg
Picha: ADEM ALTAN/AFP via Getty Images

Stoltneberg alikuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu. 

Cavusoglu hata hivyo amerudia msimamo wa Uturuki kwambahawatayatathmini maombi hayo kwa pamoja, na hasa kufuatia mvutano ulioibuka mwezi uliopita, baada ya tukio la kuchomwa Qur'an nje ya ubalozi wa Ankara mjini Stockholm.

Soma pia:NATO yajadili kuongeza kiwango cha matumizi ya ulinzi

Finland na Sweden waliomba kujiunga na NATO baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mwezi Februari mwaka jana, lakini Hungary na Uturukibado hawajaidhinisha hadi sasa.