1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SPD kuchukua uamuzi baada ya matokeo ya Dresden

25 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEXp

Berlin:

Chama tawala cha Social Democratic (SPD) nchini Ujerumani kitatangaza uamuzi wake kuhusu uwezekano wa kuundwa serikali ya mseto baada ya matokeo ya uchaguzi mdogo wa Bunge utakaofanywa Dresden. Uchaguzi mdogo huo utafanywa Oktoba 2 baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge. Mwenyekiti wa chama cha SPD, Bw. Franz Müntefering, akitilia mkazo msimamo huo katika gazeti la „Bild am Sonntag“ amekataa pia kujadili suala la nani atakuwa Kansela katika serikali hiyo. Chama tawala cha SPD na chama kikuu cha upinzani cha Christian Democratic (CDU) na chama ndugu Christian Social (CSU) vitakutana Jumatano ijayo na kuendelea na mazungumzo yao ya muungano. Vyama ndugu vya CDU/CSU na mshirika wake Free Democratic (FDP) vimepata viti 225 katika uchaguzi mkuu wa Septemba 18. Chama cha SPD kina viti 222. Kwa vile vyama ndugu vya CDU/CSU na mshirika wake FDP havina wingi mkubwa haviwezi kuunda serikali peke yao.