1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sirte, Libya. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa ayataka mataifa tajiri kuangalia suala la haki sawa ya biashara kama njia ya kuondoa umasikini katika bara la Afrika.

5 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CExB

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bwana Kofi Annan ameuambia mkutano wa viongozi wa bara la Afrika nchini Libya kuwa ana matumaini , viongozi wa kundi la mataifa tajiri duniani yenye viwanda G8 , utaangalia zaidi katika suala la haki sawa ya biashara kama njia ya kuondoa umasikini katika bara la Afrika.

Bwana Annan amesema kuwa mkutano wa kundi hilo la G8 utakaofanyika nchini scotland kuanzia kesho Jumatano unahitaji kupiga hatua kutoka majadiliano ya mkutano wa Doha wa shirika la biashara la duniani WTO.

Hii amesema , itatoa kwa wakulima wa Afrika nafasi kubwa katika masoko ya mataifa tajiri. Mwenyeji wa mkutano huo kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi amesema kuwa Afrika inalazimika kuacha omba omba na ipambane katika utatuzi wa matatizo yake.

Viongozi hao wa umoja wa Afrika wanatarajiwa kuidhinisha mpango unaoungwa mkono na Uingereza kuwa kundi la mataifa ya G8 yaongeze misaada kwa bara la Afrika na kufuta madeni zaidi.