1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKimataifa

SIPRI: Mapato ya makapuni ya uzalishaji silaha yamepungua

4 Desemba 2023

Shirika la Utafiti kuhusu Amani -SIPRI limesema mapato ya makampuni makubwa zaidi duniani ya uzalishaji silaha, yamepungua.

https://p.dw.com/p/4ZjWW
Bilder zu Story "Sipri Report"
Ripoti ya SIPRI kuhusu kupungua kwa mapato ya makampuni ya uzalishaji wa silahaPicha: Vitaliy Belousov/SNA/imago

SIPRI yenye makao yake mjini Stockholm nchini Sweden imesema katika ripoti iliyochapishwa Jumatatu  kuwa hali hiyo imeshuhudiwa  licha ya vita vya Ukraine na juhudi za mataifa mengi ya Ulaya kuongeza uwekezaji katika sekta ya ulinzi.

SIPRI imesema jumla ya mapato ya makampuni 100 mnamo mwaka 2022 ikilinganishwa na mwaka uliopita, yalipungua kwa asilimia 3.5 ikiwa ni sawa na dola bilioni 597.

Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na kuongezeka kwa mivutano sehemu mbalimbali ulimwenguni, vimesababisha kuongezeka kwa mahitaji ya silaha na vifaa vya kijeshi, lakini kulingana na ripoti ya SIPRI, kampuni za silaha kwa sasa hazina uwezo wa kutosha wa uzalishaji ili kukidhi mahitaji hayo.